TANZANIA: Kioo waja kwa kasi..
16 May 2016

Tasnia ya Sanaa ya muziki nchini Tanzania unazidi kushika kasi siku hadi siku. Baada ya muda mrefu wa maandalizi ya kuzindua albamu yao ya EP#Albamu ya ‘Nachukua Time’
“Kioo” ni wasanii chipukizi ambao kipaji chao kimejulikana kupitia Panamusiq mwaka 2015. Kioo ni jina linaloundwa na wasichana wawili ambao ni mapacha, Husna pamoja na Hawa Mkungo.
Baada ya miezi miwili ya mafunzo yao ya kimuziki waliyokuwa wakipewa na Tony Joett ambae ni mkufunzi wa muziki, walirekodi albamu yao hii ya #Nachukua Time wakiwa katika studio za C9 records, ambayo ni moja kati ya studio zinazofanya vizuri katika kutengeneza muziki hapa nchini.
Neon EP ni Extended Play albam, ambayo maana yake ni albamu yenye muunganiko wa nyimbo 3-5 au albau yenye nyimbo zisizotumia dakika zaidi ya 30.
Hizi ni nyimbo zinazopatikana katika albamu hiyo:
- Unaweza
- Nachukua time
- Love me back
- Hayana ufundi ft Dully Sykes
Unaweza kutazama baadhi ya picha zao hapa:





Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz




Leave your comment