TANZANIA: Diamond Platnum akanusha juu ya stori kuwa mama Tiffa anachepuka na Ivan

 

Star wa Bongo fleva Diamond Platnum akanusha juu ya stori zilizozagaa mitandaoni kuwa mpenzi wake Zarina ama mama Tiffa anachepuka na Ivan huku yeye akichepuka na video Quuen wa Ketu ya Raymond

Akizungumza na Enewz Diamond alisema kuwa hizo ni stori tu ambazo mapaparazi waliamua kuzitengeneza lakini Zari hakuwahi kuwa na uhusiano wowote na Ivan tangu awe na yeye.

“Mahusiano yetu ni ya kimaarufu ambayo yamempelekea hadi X wake nae pia kuwa maarufu so unapokuwa maarufu vitu vinakuwa vingi na kwa Irene wanahisi hivyo kwakua ni mzuri na kwakuwa naonekana maarufu na ninauwezo na vile pia Ray ni msanii wetu so wanahisi naweza kufanya hivyo pia.” Alisema Diamond

Stori zilizozagaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ni kuwa Zari amerudiana na mpenzi wake wa zamani na inasemekana kwa sasa Zari na Ivan wanachepuka huko South Africa wakati Mondi naye akijiachia na Irene ambae ni video Queen wa Raymond katika nyimbo ya Kwetu.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

Leave your comment