TANZANIA: Show za ndani ya nchi zinalipa zaidi kuliko zile show za nje ya nchi- Shettah

 

Msanii Shettah ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya 'Namjua' amefunguka na kusema kuwa watu siku zote hawaelewi kuwa show za ndani ya nchi zinalipa zaidi ya zile show wasanii wanafanya nje ya nchi.

Shettah amefunguka hayo kupitia kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kusema kuwa wasanii wanategemea zaidi show za ndani kuliko zile za nje kwa kuwa za ndani zinawapa mpunga zaidi.

"Unajua watu huwa hawaelewi tu lakini ukweli ni kwamba show za ndani ya nchi zinalipa zaidi kuliko zile show za nje ya nchi, hivyo hata mimi nafanya muziki wa Afrika na kuwekeza kwenye video nzuri lakini bado sijafanikiwa kuliteka soko la Afrika vizuri mpaka nikapata show za nje nyingi na kubwa. Ila nashukuru Mungu kwani kazi nazofanya matokeo yake huwa makubwa kwani ukiona unafanya kazi na hupati faida kwa sasa inabidi ujiulize na uongozi wako unakosea wapi, maana saizi biashara ya muziki ni kubwa sana", alisema Shettah

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment