TANZANIA: Achaneni na skendo, Mr Blue sasa nakuja na mambo mazuri – Mr Blue

 

Msanii wa muziki wa bongo fleva Mr Blue amefunguka na kuwataka mashabiki zake kuachana na skendo na habari zilizozagaa kwenye vyombo vya habari kwa sasa juu yake yeye na kudai kwa sasa mambo mazuri yanakuja kwani kazi yake na Alikiba imekamilika.

Mr Blue alitumia Acount yake ya Instgram kufikisha ujumbe huo kwa mashabiki wake na kuwaambia kazi ambayo amefanya na msanii Alikiba kwa producer Man Water 'Combination Sound' imekamilika na sasa ipo mikononi mwake.

"Nataka kuwaambia kuwa nawapenda sana ila nataka muachane na skendo ambazo zipo kwenye vyombo vya habari, Mr Blue sasa nakuja na mambo mazuri yanakuja"

Wiki kadhaa Mr Blue alisema kuwa wimbo wake mpya anaotegemea kuachia amefanya na Alikiba na leo amethibitisha kwa wimbo huo kukamilika na kusema muda wowote kuanzia sasa anauachia na huo ndiyo utakuwa ujio wake mpya.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment