TANZANIA: Usajili wa Nedy Music kwenye lebo ya PKP umechangiwa na uimbaji wake kuwa tofauti - Mubenga

 

Meneja wa Star wa bongo fleva anayetamba kupitia lebo ya PKP, Ommy Dimpozi, Mubenga amefunguka juu ya usajili wa msanii mpya katika lebo hiyo anayekwenda kwa jina la Nedy Music

Akizungumza na Enewz Mubenga amesema kuwa usajili wa Nedy Music umechangiwa na uimbaji wake kutofanana na wasanii wengine wanaoigana na kukopiana.

 

Mubenga

 

“Uimbaji wake tofauti na Ommy kwasababu ana kila kitu chake ana swaga zake, image yake na ana uandishi wake kwahiyo wasanii wapya wakija waje na talenti zao ili ziweze kuwapa urahisi wa wao kufanya biashara zao za kimuziki, lazima msanii mpya uwe na uwezo na uwe na kipaji chako usiimbe kama fulani fanya kitu chako hata kama huna uwezo wa kwenda studio wadau wapo watakuwezesha tu”, alisema Mubenga

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment