TANZANIA: Mo Music aweka wazi vigezo vya mwanamke ambaye anamuhitaji

 

Msanii Mo Music ameweka wazi kuwa hayupo kwenye mahusiano yoyote kwa sasa, na kuweka vigezo vya mwanamke ambaye anamuhitaji katika maisha yake.

Mo Music ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa na EATV, na kusema kuwa mwanamke anayemuhitaji awe mwenzi wake asiwe na wivu wa kumbana kwenye kazi zake, pia awe mcha Mungu.

“Awe na hofu ya Mungu asinibanebane, ajue time hii ya kazi aniachie, asiwe na wivu, awe classic”, alisema Mo Music.

Mo Music ambaye amekiri kazi zake nyingi anazifanya kutokana na maumivu ya mapenzi aliyoyapata kutoka kwa mwenzi wake aliyeachana naye akiwa chuo, na kusema mara nyingi akiandika nyimbo huwa anamkumbuka.

“Nishawahi kuumizwa, unajua mi nilikuwa na mwanamke wangu, nilianza ku-date naye nikiwa form two mpaka mwaka wa kwanza, ye alikuwa ndo anamaliza form six, hizo pain mpaka leo zina-click kwenye kichwa changu, lakini ndio zinanifanya niweze kufanya vizuri kwenye muziki, na kwa sasa tumebaki marafiki tu”, alisema Mo Music.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

Leave your comment