TANZANIA: Ney wa Mitego sio msanii mkali - Kimbunga Mchawi

 

Msanii Kimbunga mchawi amemuwakia msanii mwenzake Ney Wa Mitego, na kusema kuwa hawezi muziki.

Kimbunga ameyasema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Enews kinachorushwa na East Africa Television, na kusema kuwa hawezi hata kufanya naye kazi kwani hajui kabisa muziki.

 “Msanii Ney wa Mitego sio msanii mkali, hajui nguzo za hip hop, hajui muziki hata aimbe wimbo gani hawezi, na siwezi kumshirikisha na sijawahi kushirikiana naye, yeye ndo aliwahi kunishirikisha kwenye nyimbo zake, na kwasababu kulikuwa na wasanii wengine kama kina baghdad, nikaona kazi nzuri nami nikakubali”, alisema Kimbunga Mchawi.

Hivi karibuni Msanii Ney wa Mitego alikuwa gumzo kwenye midomo ya watu, baada ya kutoa wimbo uliowaponda wasanii wenzake, na kupelekea BASATA kuufungia.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment