TANZANIA: Nimekamilisha albam yangu, na nitaipa jina la mwanangu ‘Mali’- Ben Pol

 

Msanii wa muziki wa R&B, Benard Paul ‘Ben Pol’, yupo katika maandalizi ya mwisho ya kuachia albamu yake aliyoipachika jina la mwanaye wa kwanza, ‘Mali’ aliyezaliwa hivi karibuni.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania, Ben Pol amesema albamu hiyo itatoka katikati ya mwezi wa sita.

“Nimefanikiwa kukamilisha albamu yangu bila msaada wa mtu mwingine yeyote ndiyo maana nimeamua kuiita jina la mwanangu, ‘Mali’. Kwa sababu kila kitu nimefanya mwenyewe na kuenzi jina la mwanangu,” alisema Ben Pol.

Pia Ben Pol alisema kabla ya kuachia albamu hiyo anatarajia kuachia video ya wimbo ‘Moyo’ akiwa ameifanyia nchini Afrika Kusini chini ya mtayarishaji, Lolpop katika studio ya Tetemesha.

 

Leave your comment