TANZANIA: Diamond na Mafikizolo ndani ya UDOM, alhamisi hii…
10 May 2016

Kampuni ya Vodacom Tanzania itawaleta wasanii wa Afrika Kusini, Mafikizolo kwenye show ya pamoja na Diamond Platnumz kwenye chuo cha kikuu cha Dodoma, UDOM Alhamis hii.
Show hiyo ni sehemu ya matamasha yanayoandaliwa na kampuni hiyo vyuoni ambayo humhusisha Diamond ambaye ni balozi wake. Mafikizolo walimshirikisha hitmaker huyo kwenye wimbo wao ‘Colors of Africa.’ Hiyo inakuwa takriban mara ya tatu kundi hilo kutua nchini.
Katika akaunti yake ya Instagram Diamond alipost na kusema kuwa: DODOMA!!! DODOMA!!! UDOM! UDOM!! UDOM!! alhamis hii ya tareh 12 @VodacomTanzania inakuletea @DiamondPlatnumz pamoja na MAFIKIZOLO toka South Africa hapo chuoni UDOM kukupa BURUDANI ambayo Haitokaa itokee... narudia tena, Haitikaa itokee!... tafadhali nisaidie kuwatag ili kuwajuza wana Chuo woooote wa hapo na vyuo vingine... halaf sasa, kiingilio buuuuuuuureeeeeee....... It's all About Colors of AFRICA!!!! #ColorsOfAfrica link in my BIO!!!! @theoMafikizolo @nhlanhla_Nciza #VodacomKaziNiKwako #VodacomOngeaDeilee




Leave your comment