TANZANIA: Nitatumia njia ya sanaa kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa mpana juu ya ugonjwa wa UKIMWI – Mrisho Mpoto

 

Ugonjwa wa Ukimwi ni sababu kwanza inayopelekea vifo vya vijana wengi barani Afrika wenye umri wa kuanzia miaka 15 mpaka 24 wengi wao wakiwa ni wasichana jambo ambalo linazidi kuwafanya wadau wakupambana na ugonjwa huo kutumia mbinu mbalimbali za kutoa elimu kwa jamii hasa vijana kuepuka maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika uteuzi wa Balozi wa Kilimanjaro HIV/AIDS Chalenge iliyofanyika kwa miaka 16 sasa na mgodi wa dhahabu wa Geita kwa lengo la kutoa elimu juu ya ugonjwa huo Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti na Kupambana na Ukimwi nchini TACAIDs Dk. Fatma Mrisho amesema, takwimu zinazofanywa kila baada ya miaka 4 juu ya VVU inaonyesha kuwa mpaka sasa Ukimwi umepungua kwa asilimia 5.8 kutoka asilimia 7.1 mwaka 2007 lakini kundi la vijana liko kwenye hatari zaidi.

Naye Balozi mpya wa Kili Chalenge msanii Mrisho Mpoto amesema, atatumia njia ya sanaa kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa mpana juu ya ugonjwa huo hasa vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa na kuwataka wanajamii kwa pamoja kupambana na ugonjwa huo unao didimiza uchumi wa taifa.

“Nashukuru kupata nafasi hii ili kuweza kutoa mchango wangu katika kusaidia jamii kuepukana na janga linalotokana na maambukizi ya VVU, nitatumia sanaa yangu ndani na nje ya nchi kuhakikisha kuwa Ukimwi unamalizika kama lengo la viro 3 linavyolenga,” alisema Mpoto.

Kilimanjaro Challenge ni mradi unaolenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu ugonjwa wa Ukimwi na Virusi vya Ukimwi pia inalenga kuchangisha fedha ili kujenga timu imara itakayo endeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

 

 

Leave your comment