TANZANIA:Cover ya Aza ilinisabibishia nifungwe – Bonge la Nyau

 

Msanii Nyauloso maarufu kama Bonge la Nyau amesema cover ya kwanza ya wimbo wake mpya ‘Aza’ lilimsababishia atake kufungwa.

Hili ni kava la awamu ya pili baada ya lile la mwanzo kumletea kesi

Akiongea kwenye kipindi cha E News cha EATV, Nyauloso alisema ‘ile picha ya yule msichana iliyoonekana kwenye ile cover ya mwanzo ilinisababishia matatizo makubwa.’

“Poster yangu ya wimbo wangu mpya yule aliyenitengenezea, director Khalfan alimchomeka msichana, ukiangalia utamuona. Yule msichana alisema zamani alikuwa model, aliponipa ile cover niliuliza iko sawa? Wakanambia iko sawa lakini niliipenda kwa sababu ilikuwa na muonekano mzuri nikaipost,” aliongeza.

Aliendelea, “Baada ya kupost yule demu akaanza kunipigia simu sikupokea kwa kuwa ilikuwa namba mpya, ikaingia simu nyingine nikapokea alikuwa ni mwanasheria. Nikapokea akanambia atanifunga na ataliletea summons. Walinisamehe lakini walichoniambia niwapigie simu watu wote walioipost waifute halafu ndiyo tutakusamehe. Nikawapigia simu wadau wote kwenye muziki nikawaelezea ilivyokuwa wakanielewa wakafuta,” alisema.

Katika hatua nyingine Nyauloso kwa sasa hafanyi tena kazi na producer aliyemtambulisha kwenye muziki wa Bongo Fleva, Bob Junior kwa taarifa za kuwa wamegombana na sasa anafanya kazi na producer Ammy Tiger.

 

 

Leave your comment