TANZANIA: Niliwachukua wanawake wenzangu kucheza na si kuwadhalilisha - Snura

 

Msanii Snura ambaye jana video ya wimbo wake wa 'Chura' ulifungiwa na serikali kutokana na kutokuwa na maadili na kukiuka utamaduni wa kitanzania amefunguka na kusema kuwa yeye kukata viuno amejifunzia kwenye ngoma za asili.

Snura ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ambapo alikuwa akitoa ufafanuzi na kuomba radhi kwa watanzania kutokana na video yake hiyo kutokuwa na maadili na kuwadhalilisha wanawake.

"Mimi ni mwanamke na niliwachukua wanawake wenzangu kucheza lakini haina maana kuwa niliwachukua ili niwadhalilishe hapana, ila nakiri kuwa nilichokosea ni kuwaingiza kwenye maji ndiyo maana ilionekana kama ni udhalilishaji kwao. Lakini kucheza hakumdhalilishi mtu na ndiyo maana kuwa bendi wachezaji show wake wanakatika hata kwenye ngoma zetu za asili tunakatika, mimi nimejifunza kukatika kwenye ngoma za asili kwani ndiyo kipaji changu cha kwanza na huko ndiyo nimejifunzia kiuno" alisema Snura

 

 

Leave your comment

Top stories

More News