TANZANIA: Maisha ya umaarufu magumu sana- Dudubaya

 

Msanii Dudubaya amefunguka na kusema kuwa maisha ya kuwa maarufu ni magumu sana kwani kuna wakati unashindwa kufanya vitu ambavyo wewe unapenda kutokana na kuwa na umaarufu.

Dudubaya kupitia kipindi cha Planetbongo amekiri kuwa kuna wakati anajutia maamuzi yake ya kutaka kuwa maarufu na kuwa maarufu kwani yanamfanya aishi maisha ambayo si yake kwani akifanya vitu vingine baadaye vinageuka stori mitaani na mitandaoni.

"Kuna wakati huwa nasema kwanini nilitaka kuwa star na nikawa star kwa sababu kuna wakati mwingine unatamani kufanya jambo fulani lakini unashindwa kufanya kutokana na umaarufu wako, maisha ya umaarufu magumu sana haya mambo yanatukuta hata mtaani mfano unaweza kuwa unakaa uswahilini unakaa Manzese, Tegeta, Mwananyamala mtu mwingine anaweza kukudharua kumbe ni maisha ya kawaida kama watu wengine. Mfano mzuri mimi napenda sana mihogo na vitumbua lakini nashindwa kwenda kununua mtaani kwani nikisema niende tayari watu wanaleta skendo mtaani," alisema Dudubaya.

Dudubaya anaonyesha kuwa maisha ya kuwa maarufu ni mzigo mzito kama ambavyo Fid Q alishawahi kusema kuwa 'u Superstar' ni mzigo wa mwiba ukiubeba utaumia.

 

 

Leave your comment