TANZANIA: Niliwahi kumpa gari mwanamke wangu kwa kumjali – Nay wa Mitego

 

Msanii Nay wa Mitego amefunguka na kuweka sawa kuwa yeye ni mtu ambaye anajali sana hasa pale anapopata mtu ambaye anampenda na suala la yeye kumpa mwanamke kitu au huduma ni jambo la kawaida.

Nay wa Mitego amesema haya kupitia eNewz wakati akitoa ufafanuzi juu ya maelezo aliyoyatoa msanii wa filamu Niva Supermario ambaye alidai kuwa Nay wa Mitego aliachwa na Shamsa Ford sababu hajui kuhudumia na alikuwa akimpiga sana virungu Shamsa Ford.

"Unajua watu hawajui tu lakini nataka kumwambia huyo bwana mdogo Niva mimi niliwahi kutoa gari ya kwangu ya kutembelea na kumpa mwanamke wangu sababu tu nampenda na kumjali," alisema Nay wa Mitego.

 

 

Leave your comment