TANZANIA: Ben Pol afunguka kuhusu mwanaye, na apewa jina la ‘Magufuli’
3 May 2016

Msanii wa RnB Nchini Ben Pol amefunguka kuhusu Mtoto aliyempata hivi Majuzi kwa Kutusanua Jina Lake na Maana ya Jina la Mwanaye.
Ben Pol ametufungulia jina la Mwanaye mwenye Umri wa Mwezi mmoja na nusu kwamba anaitwa Mali, Maana ya jina hilo ameielezea kwamba ni Kuonyesha Thamani kwakuwa wanasema Majina yanaumba kwa hiyo Kumuita Mali ni Njia ya Kumtabiria Mwanaye.
Jina la Pili la Mwanaye ni Magufuli ambalo amepewa na Baba yake kwakuwa amezaliwa Kipindi hiki ambacho Rais Magufuli ana-Trend.
Kwenye Point ya Msingi Ambayo unatakiwa kuidaka ni kwamba Ben Pol na mpenzi wake Wamempata mtoto huyu Kabla za Kufunga Ndoa na Ben Pol ametujibu kwanini akapata Mtoto nje ya ndoa kwa kusema kuwa kwa upande wake Mwanamke Akipata ujauzito Haoni njia myingine zaidi ya Kuzaa.
Chanzo: VMG Africa




Leave your comment