TANZANIA: Producer ‘Magulu pande’ alivutiwa na mimi kupitia ‘Vuvula’

 

 

Madee amesema producer huyo alimsikia kwenye nyimbo ya Vuvula na kupenda uimbaji wake, hivyo alifanya mpango wa kuwasiliana kwa kumtumia Babu Tale, na kurekodi wimbo huo.

“Producer alivutiwa na mimi baada ya kuona vuvula, akamwambia Babu Tale kwa sababu wanafahamiana, akamtumia Babu Tale beat kama nne, katika hizo beat nikaipenda hiyo, akaituma, na mimi nikatuma vocal akafanya mixing, ila mastering ndio amefanya Tud Thomas”, alisema Madee.

Pia Madee amezungumzia mipango ya kuachia ngoma yake aliyofanya na Tekno, na kusema kazi hiyo inahitaji jitihada zaidi kabla ya kuitoa, ikiwemo kufanya video nzuri.

“Nimeshafanya na Tekno, ila inatakiwa tujipange kwanza video kubwa na vitu vingine, sasa kati kati hapa Tekno alikuwa busy sana Marekani, so tukaona tukisubiri tena tutachelewa, tukaona tutoe hii kwanza na kisha hiyo itafuata”, alisema Madee.

 

Chanzo: Bongo5

 

 

Leave your comment

Other news