TANZANIA: Dogo Janja ajibu shutma za kuiba beat la ‘My Life’

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dogo janja amesema yeye si wa kwanza kuitumia beat hiyo, na pia watu wanatakiwa waelewe kuwa beat sio mali ya msanii bali ni mali ya producer, na anaweza akampa mtu yeyote kuitumia.

“Ile ngoma kaitengeneza producer kutoka Norway, na yule ni msanii wake, na pia sio mimi tu nitakayeitumia beat ya my life, Gyptian wa Jamaica ameshaanza kuifanyia kazi” alisema Dogo Janja.

Pia Dogo janja amesema beat hiyo wana plan ya kutengeneza albam ya nyimbo zilizotumia beat hiyo, na kumpa chance ya kuwa msanii pekee kutoka Afrika aliyetumia beat hiyo, huku akitoa siri ya kurekodi nyimbo ya My life.

“Vile vile inatengenezewa albam ya ile beat, na Afrika ndio mimi nimeipata, halafu kama unakumbuka ilibidi nika-rekodie Norway audio na video ila passport yangu imepotea mpaka leo sijaipata, so jamaa akashuka tukairekodia bongo”, alisema Dogo Janja.

 

 

Leave your comment