TANZANIA: Sijaacha muziki - Cpwaa

Rapper Cpwaa amesema ukimya wake haumaanishi kuwa ameacha muziki. Ameiambia Bongo5 kuwa katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni amekuwa akifanya shughuli zake binafsi zinazohusiana na fani ya IT aliyoisomea.

Amedai kuwa katika kipindi hicho pia amekuwa akirekodi nyimbo kibao huku sasa akijiandaa kufanya video na muongozaji wa ndani. “Siwezi kurudi kwa style ile ile ya kizamani au kwa strategy zile zile, game imebadilika sasa hivi, watu wako vizuri, wanafanya kazi nzuri,” amesema.

“Nipo kwenye hatua pia ya kuweza kurudi kwenye style ambayo itaweza kwendana na ushindani ambao upo kwa sasa,” ameongeza.

Rapper huyo amesema mashabiki wake wamekuwa wakimuuliza karibu kila siku kwenye mitandao ya kijamii na sehemu zingine kuhusu ukimya wake na amekiri hilo kumsumbua.

“Ni kitu ambacho kinanikwaza sana, nakaa na watu kwenye mamall nikitoka wanauliza ‘bana vipi mbona umeacha, hebu rudi.’ Challenge ambayo nakutana nayo sasa hivi najiuliza kwenye video labda nifanye na nani. Siwezi kudanganya, siko tayari kutumia $40,000 sasa hivi niende South Africa kufanya video wakati nina majukumu mengi. Kwahiyo siwezi kuchukua hela yangu inayoniingizia mkate wangu wa kila siku kuipeleka huko,” amesisitiza.

“Lakini I promise the industry mpaka kwamba by June watakuwa tayari wameshapata mzigo wangu mpya kabisa.”

 

Chanzo: Bongo5

Leave your comment