TANZANIA: Bado sijamaliza soko la muziki wa Tanzania – Kala Jeremiah

 

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Kala Jeremiah amesema hawezi kuangaika kwenda kimataifa kwa sasa kwa kuwa bado hajalimaliza soko la muziki wa Tanzania.

Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Kala amesema kwa sasa amewafikia robo ya Watanzania wote.

“Kwa haraka haraka bado Watanzania wanahitaji huduma yangu, bado nachangamoto ya kuweza kuwafikia Watanzania wengi zaidi, kwa hiyo kabla sijaenda nje nahakikisha kwanza nimelifikia kwanza soko la Watanzania,” alisema Kala.

Pia Kala amesema wasanii wengi ambao wamefanya video nje kwa malengo ya kwenda kimataifa wameshindwa kufikia malengo hayo.

“Wasanii ambao wameenda kushoot video zao nje niwachache wamefanikiwa kutoboa katika mataifa ya watu, wawili au mmoja. Kwa hiyo bado kuna changamoto unaweza kufanya video ya milioni 40 na isifike kule unakohitaji, na bado tunaenda wote kwenye show za Mwanza na Iringa, yaani unakuwa kama msanii wa kawaida ambaye video yake amefanyia hapa, kwa hiyo wasanii tunatakiwa kujiangalia kabla kufanya hivi vitu,” alisema Kala

 

Chanzo: bongo5

Leave your comment