TANZANIA: Snura azungumzia wimbo yake ya Chura

 

Zimepita siku tatu tangu kuachiwa kwa video ya Chura ya msanii “Snura” wakati audio ya wimbo huo ikiwa gumzo kutokana na watu wanavyojirekodi wakiucheza wimbo huo kwa staili tofauti imefanya mahojiano na Meneja wa msanii Snura Hemed Kavu maarufu kama HK ambapo amefunguka kuhusu maana ya wimbo huo na kuhusu video hiyo ambayo inaonekana ipo nje ya maadili.

“Wimbo wa Chura umelenga watu ambao wana mchezo wa kuruka ruka katika mapenzi unakuta leo upo na huyu kesho upo na yule ndio watu ambao tumewagusa kwenye wimbo wa Chura, mwanaume au mwanamke asiyetulia katika mapenzi huyo ni Chura”

Akizungumzia kuwepo kwa video inayotajwa kutokuwa na maadili HK amesema video hiyo imetolewa kama bonus track na wimbo imetolewa maalum kwa mitandao ya kijamii na sio maalum kwa kuchezwa kwenye vituo mbalimbali vya habari.

 

 

 

Leave your comment

Top stories

More News