TANZANIA: Barnaba Classic na mipango ya kutoa albam iitwayo 88

Msanii mwenye sauti ya mvuto Barnaba clasic, ameamua kuvunja ukimya kwenye kazi zake, na kuwapa habari njema mashabiki wa muziki wake.

Barnaba ametoa habari hizo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa hivi karibuni anatarajia kutoa albam, ambayo itabeba kazi nzuri kwa mashabiki wake.

“Mwaka huu nina plan ya kutoa albamu, iko plan tayari good news albam yangu inaweza ikaitwa 88, sababu na kwanini nimepelekea kuita 88 kwa sababu tarehe 8 mwezi wa 8 sikukuu ya wakulima, lakini pia albam yangu inaweza ikawa na nyimbo nane ndani yake, na naweza nikaitoa tarehe nane mwezi wa nane, lakini kabla haijatoka kuna wimbo nimeu-release unaitwa wanifaa, na ni one of the song ambayo itabeba albam yangu au itasindikiza 88”, alisema Barnaba.

Pia Barnaba ameelezea ukimya ambao alikuwa nao kwenye kazi zake, na kuhusu suala la kutoa video ya wimbo wa Nikutunze aliofanya na msanii kutoka Uganda Jose Chameleone.

“Nimekaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa nyimbo yoyote ile tangu nimetoa albam zangu mbili zilizopita, lakini hapa kati kati nimefanya collabo kubwa na msanii mkubwa wa East Africa Jose Chameleone, video ilichelewa kutoka kutokana na mipango ya hapa na pale na mambo yaliyokuwa nje ya uwezo wangu, haikuwa kwa ubaya lakini video hiyo itakuja kufanyika, nina ratiba zinaendelea kwa sababu safari hii nimebadilisha uongozi kidogo, menejimenti imeongezeka, kuna watu wameongezeka ndani yake”, alisema Barnaba.

 

Leave your comment