TANZANIA: “Video ya Chura ni maalum kwa ajili ya YouTube na sio Tv” - Snura

Msanii wa muziki wa bongo fleva Snura Mushi ametoa video yake hivi karibuni ambayo ilifanyiwa uzinduzi siku ya tarehe 24 April katika viwanja vya Maisha basement na kuhudhuriwa na watu wengi. Mapokeo ya video hiyo yamekuja kwa hisia tofauti. Kuna wanaoipenda na kuna wanaoiponda.

Katika kuliona hilo Snura aliliongelea kupitia mahojiano yake na Millad Ayo na kusema kuwa video yake aliitoa mahsusi kwa ajili ya YouTube na sio kwa ajili ya tv za kawaida.

Snura alisema: “Kiukweli video ya Chura nimeifanya maalum kwa ajili ya youtube na wala sina mpango wa kuipeleka kwenye Tv yoyote Tanzania, licha ya kuwa nimetumiwa taarifa kuwa Kenya imeshaanza kuchezwa, kwa wanaosema haina maadili mimi sijaitengeneza kwa ajili ya Tv bali youtube kwa anaependa kuitazama ataitazama na kwa mtu ambaye kwake haina maadili asiingie youtube kuiangalia”.

Unaweza kuiangalia video hii hapa:

Leave your comment