TANZANIA: Albamu yangu ya 'Sweety Sweety' itaanza kuuzwa kwenye matamasha - Chegge

 

 

Mkali wa ‘Sweety Sweety’, Chege Chigunda amesema tayari amekamilisha maandalizi ya kuiingiza sokoni albamu yake mpya ya ‘Sweety Sweety’.Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Chege amesema albamu hiyo itaanza kuuzwa kwenye matamasha kabla ya kuwekwa katika maduka mbalimbali.

“Maandalizi ya albamu yamekamilika kabisa, nitaanza kuuza albamu yangu kwenye matamasha mbalimbali mbayo nitakuwa nayafanya, na baadae ndio itaanza kupatika katika maduka mbalimbili,” alisema Chege.

Aliongeza, “Unajua hata ulaya licha ya kuuza kazi zao kwa mifumo yao, lakini pia wanategemea kuuza kazi zao katika show zao. Kwa hiyo kwa upande wangu nimeona hii ni fursa kwangu kuweza kuuza albamu yangu,”

Chege amewataka mashabiki wa muziki kuisubiria kwa hamu albamu hiyo kwa kuwa imesheheni kazi nzuri pamoja na kolabo.

 

Chanzo: Bongo5

Leave your comment

Other news