TANZANIA: Mimi naamini kipaji changu na siyo upepo wa muziki – Mo Music
27 April 2016

Msanii wa Bongo Fava Mo Music amesema kwamba kukaa kimnya kwa muda imesababishwa na kutokuwa na 'management' ambayo ingewezesha yeye kuweza kutoa video kali kwa sasa.
Msanii huyo aliyetamba sana ngoma yake ya Basi Nenda ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano maalum katika kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na EATV.
Kuhusu kubadilika kulingana na upepo wa muziki ulivyo kwa kubadili namna ya uimbaji msanii huyo amesema yeye haamini katika upepo wa muziki bali anaamini kipaji chake ndicho kitakacho mtoa.
''Mimi naamini kipaji changu na siyo upepo wa muziki japo nimebadili kidogo katika nyimbo nyingine ila lengo ni kuweza kuwapa mashabiki wangu vitu ambavyo wanavitaka''- Amefunguka Mo Music.




Leave your comment