TANZANIA: Aika aelezea sababu ya yeye na Nahreel kutoka kwenye kundi la Pah one

 

Kabla ya kundi la Navy Kenzo kuwepo, walikuwa katika kundi liitwalo Pah One lakini walikuja kutengana na kuunda kundi lao liitwalo Navy Kenzo.

Katika mahojiano ya Aika na Mdundo.comalielezea sababu zilizpelekea mpka wakatoka kwenye kundi hilo la Pah One.

“Hakukuwa na maelewano kati ya pande mbili, wawili walikuwa ni ndugu na kwa upande mwengine mimi na Nahreel tulikuwa tunadate lakini hata hivyo haikuwa ndio sababu ya sisi kutengana. Sababu kubwa ni kwamba tulikuwa tunatofautiana katika fikra zetu upande wangu na Nahreel pamoja na upande wao.”

“Walikuwa wanasema wao ndio mastaa kuliko sisi na wao ndio waliokuwa wanamchango kubwa kwenye muziki.” Aliongeza Aika. Aika na Nahreel hawakukata tamaa katika muziki na wakazidi kupambana.

Aliendelea Aika na kusema, “Tukatoa nyimbo mimi na Naheel inaitwa “Usinibwage”. Kwakuwa tumekuwa pamoja tangu mwaka 2008 hatujawahi kuwa na tatizo kwahiyo tukaona kwanini tukate tamaa, tukaona tuform a group na tuendeleze muziki ambao tulikuwa tumeuanzisha. Tukaja na jina la Navy Kenzo, Kenzo ikiwa na maana watu shupavu,wanyenyekevu na Army kama inavyojulikana ni wanajeshi, kwahiyo tukaona tujiite Navy Kenzo”

Kwasasa kundi la Navy Kenzo linaendelea na tour yao iitwayo Kamatia Tour, Lights Up Tour ambayo wameenda maeneo tofauti kama Dodoma, Morogoro, Iringa na Nairobi.

Leave your comment