TANZANIA: Barnaba awapotezea majirani zake
25 April 2016

Baada ya cheche kumdondokea msanii wa Bongo Fleva Barnaba na majirani zake kumponda star huyo ameonesha wazi kutojali tuhuma hizo dhidi yake na kuamua kuzitupilia mbali.
Hivyo kupitia Enewz Barnaba amewataka mashabiki zake wakutane Jumapili hii Tegeta kwenye miaka 17 ya East Africa Radio ili wawe wa kwanza kusikia wimbo wake mpya atakao uachia wiki ijayo kupitia Radio hiyo
Awali wakizungumza katika cheche ya Enewz majirani wa star huyo walidai kuwa Barnaba ana tabia ya kuwageuza vimada wasanii wa kike wanaofika ofisini kwake kuomba msaada wa kimuziki ili watoke.




Leave your comment