TANZANIA: Mama mtoto wa Nay Wa Mitego ahukumiwa miaka 2 jela.

Mahakama kuu ya mkoani Mwanza imemuhukumu Siwema ambaye ni mzazi mwenzake na Nay Wamitego miaka miwili jela kwa kesi ya kumtukana mtu kwa njia ya mtandao.


Siwema alituhumiwa kumtukana matusi kwa njia ya mtandao mlalamikaji ambaye anafahamika kwa jina la Deo. Akizunguza na kipindi cha Jahazi, kinachoruka kupitia Clouds FM, Nay Wamitego alisema ‘napambana kile nitakachoweza kuangalia kama kunauwezekano wa kumpa msaada’.


“Kuna vitu nafikiria kuvifanya ili kujaribu kumsaidia, baada ya kupata hizi taarifa kidogo kama siko sawa hivi. Ni mzazi mwenzangu mimi nay eye tulikaa muda mrefu, napambana kile nitakachoweza kuangalia kama kunauwezekano wa kumpa msaada mwingine kwa njia yeyote ili asiwe kwenye mazingira ambayo tayari ameshawekwa. Anayemshtaki najua anaitwa Deo, jina jingine silifaham,” aliongezea.


Nay na Siwema walifanikiwa kukaa kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu na kufanikiwa kupata motto mmoja, Curtis kabla hawajachana na kila mtu kushika njia yake.


Chanzo: Bongo5

Leave your comment