TANZANIA: Diamond, Mrisho Mpoto watajwa bungeni
21 April 2016
Kikao cha tatu cha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 kimeendelea tena Dodoma leo April 21 2016 , shughuli nzima iliyoanza asubuhi ni maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, Pia baadhi ya Wizara zilihusishwa katika maswali hayo, ambapo Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara hizo walilazimika kuyatolea majibu.
Baadhi ya Wizara hizo ni pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambapo swali lililoulizwa na Mbunge wa Kasuru Mjini Daniel Nsanzugwanko ilikuwa ‘Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwekeza kwakiwango kikubwa katika Mkoa wa Kigoma kwa kujenga jumba la sanaa ili vijana wawe na sehemu nzuri ya kujiendeleza kisanaa?’
Swali la pili likawa ‘Kama Serikali inakubaliana na hoja hiyo, kituo hicho kitaanza kujengwa lini?’
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akajibu ‘Wizara yangu inatambua mchango mkubwa wa wasanii wenye asili ya mkoa wa Kigoma kama vile Diamond, Alikiba, Banana, Mrisho Mpoto na wengine‘
‘Wizara yangu inaendelea kuhimiza Halmashauri na Manispaa zote nchini kutenga maeneo ya kujenga vivutio vya sanaa. Kuhusu mkoa wa Kigoma, tunashauri Serikali ya mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri zote kutekeleza ujenzi wa jumba la sanaa ‘
Leave your comment