TANZANIA: Nataka nimuoe Vanessa ndoa kabisa - Bright

 

Msanii chipikizi wa nchini, Bright anasema ana ndoto kubwa ya kumuoa diva huyo ambaye ni mwandani wa msanii Jux, huku akiweka wazi kuwa Jux hamuogopi kwani hajamuoa.


“Nampenda sana natamani kumuoa ndoa kabisa, unajua msicheke ni kitu ambacho naongea niko serious kabisa, natamani kumuoa kabisaa, ni mwanamke mzuri mwenye mvuto, mwanaume yoyote aliyekamilika lazima atamani”, alisema Bright.


Mtangazaji wa kipindi hiko Dulla alipomuuliza kuhusu itakuwaje iwapo Jux akijua, alijibu kwa kujiamini kuwa hana wasi wasi kwani Jux hajamuoa Vanessa, na yeye anataka kumuoa kabisa awe mke wake wa ndoa,


“Niko kwenye process hata kama Jux yupo naye, hawajaoana nina nafasi ya kumwambia nikamvisha pete ndoa kabisa, na sio namsubiri amuache, naweza nikamnyang'anya braza, mpaka sasa hakuna aliyetangaza ndoa kwa V Money”, alisema Bright.
Pamoja na hayo yote Bright amesema wimbo huo anau-dedicate kwa Vanessa, akimtaka amtunzie ili amuoe, huku akiwataka mashabiki kumuunga mkono kwa kuomba nyimbo yake ipigwe kwenye radio.

Leave your comment