TANZANIA: Hakuna maprodyuza wazuri Zanzibar – Sultan King

 

Msanii Sultan King anayesifika kwa kufanya vizuri kutoka pande za Zanzibar amedai kwa sasa hakuna Producer wazuri visiwani humo.

Katika mahojiano yake na Dulla kutoka katika kituo cha utangazaji wa Planet Bongo Sultan King amesema kuwa visiwani humo hakuna maprodyuza wazuri.
“Hakuna maprodyuza wa kutosha ambao wanaweza kufanya, ambao mimi nataka. Ila alikuwepo prodyuza ila kwa sasa yupo huku alamain, yeye mwenyewe amesema Zanzibar tuondoke. Na mimi hicho kitu nilitaka kubishana. Kwasababu unajua mtu unaweza kufanya kitu kizuri kokote na kitatambulikana. Mimi nilitaka nifanye muziki nyumbani na nijulikane dunia nzima” alisema Sultan King.

Unaweza kutazama hapa video ya msanii Sutan King iitwayo  'Shikilia':

Leave your comment