TANZANIA: Ningependa kufanya muziki na Collo – Mansu-li


Msanii wa miondoko ya hiphop Mansoor Ally almaarufu kama Mansu-li amesema kuwa msanii anayependa kufanya naye muziki Afrika Mashariki ni Collin Majale a.k.a Collo kutokea Kenya ambaye anafahamika pia kama king wa rap.


Mansu-li alisema hayo katika mahojiano yake na mwandishi wa Mdundo.com mara baada ya kuhojiwa kuwa ni msanii gani wa Afrika ya Mashariki angependa kufanya naye kazi, alijibu na kusema, “Msanii ambaye ningependa kufanya naye ngoma ni Collo King wa rap kutokea Nairobi Kenya, namkubali sana. Yuko vizuri kwenye kazi yake, natumai ikaja ikatokea tukafanya kazi wote tutatengeneza ngoma nzuri sana”. Ikaja kutokea Mansu-li akaja kufanya ngoma pamoja na King wa Rap kutokea Kenya, Collo watafanya kibao kikali sana kwani wote ni wakali katika muziki huu wa hiphop.

Siku chache tu zilizopita msanii huyu alitoa kibao chake kipya kiitwacho One-Two (OldSkul Vibe), kama umepitwa na kibao hiko unaweza ukakipata hapa:

mdundo.com/song/51404

Leave your comment