TANZANIA: Sijawahi kuendesha gari ya mtu – Baraka Da Prince

Msanii wa muziki wa bongo fleva Baraka Da Prince amejikuta akipatwa na tetesi ya kwamba magari anayotumia si ya kwake na kuwa anagongea kwa marafiki.
Akipiga stori na eNewz Baraka amekanusha kashfa hizo na kusema kuwa wanaosema anagongea magari ni machizi tu. Zaidi Baraka ameongeza kuwa yeye anamiliki magari zaidi ya moja na hajawahi kuendesha gari ya mtu.

Pia Baraka hakuficha kuwa kwa sasa amekwisha mtambulisha msanii mwenzake Naj kwa wazazi wake kuwa ndiye mchumba wake, na amemvisha pete ya ahadi kuwa atakuwa naye milele daima. Alipoulizwa kuwa pete hiyo inamaanisha ana nia ya kumuoa Naj, Baraka alisema “Kwa hilo Mungu ndiye anayejua”.

Leave your comment