TANZANIA: “Nguvu ambayo nimeiweka kwenye muziki wangu ime-deliver zaidi ya 800”- Belle9
19 April 2016

Msanii Belle 9 ameelezea furaha yake baada ya kufanya show ya kusherehekea miaka 17 ya East Africa Radio Gongo la mboto DSM, na kusema kuwa shangwe alizoonyeshwa na mashabiki zinamfanya aamini ana deni kwa mashabiki zake.
Belle 9 ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa nguvu aliyoitumia kuwekeza kwenye muziki inampasa aiongeze ili kulipa deni la mashabiki wake.
“Nguvu ambayo nimeiweka kwenye muziki wangu ime-deliver zaidi ya mara mia 8, zaidi ya ambavyo nimetegemea, responding ya watu imekuwa kubwa zaidi, 'for me I think' watu bado wananidai muziki, kwa sababu ile vibe nailipaje, naona sasa watu wako live kiasi gani, maana yake natakiwa nguvu niliyoiweka natakiwa niiweke mara mia 8 yake tena”. Alisema Belle 9.
Pia Belle 9 ameishukuru East Africa Radio kwa kumpa fursa hiyo, na kusema kuwa anajihisi mwenye bahati, na pia imemfungulia milango zaidi ya biashara kwake.
“Kwangu mimi najiona ni msanii ambaye nimepata bahati kubwa, huwezi amini huku ndio leo mimi nakuja, sijawahi kuja Gongo la mboto, nimepata exposure nimejua kwamba kuna watu Gongo la Mboto wanamuelewa Belle kwa level ile pale, kwangu mimi nimechukulia kibiashara hata kama kuna plan kubwa it means naweza nika-organize kupitia East Africa” alisema Belle 9.




Leave your comment