TANZANIA: Mansu-li aielezea nyimbo yake mpya ya One-Two(OldSkul Vibe)

 

Mansu-li ni msanii wa hip hop nchini Tanzania, na amekua akifanya vizuri katika tasnia hiyo. Mansu-li alishawahi kutoa nyimbo kama vile ‘Kina Kirefu’, ‘Tuko Pamoja’, ‘Inavyokua ft Godzilla”na nyinginezo nyingi. Hivi karibuni msanii huyo alitoa kibao kiitwacho ‘One-Two(OldSkulVibe) aliyoshirikishana na Zaiid.

 

Katika mahojiano yake na mwandishi wa Mdundo.com akiielezea nyimbo hiyo, Mansu-li alisema, “Kitu ambacho kiliniinspire hasa kuifanya hii ngoma, kwanza niliicheki game nikaona hiyo type ya music iko missed na watu. Hasa ukizingatia lile rika flani, watoto wengi wa kisasa sasa hawa wanaweza wasielewe'.

"Tunazungumzia hip hop ya golden era ya 1995, walikuwa wakienda klabu wanaenda kucheza hayo mangoma kwahiyo nikaona hatuwatendei haki, kwasababu kila msanii wa sasa wa hip hop amejaribu kufanya muziki wa kisasa zaidi, kuswitch floor na nini. Na hata zile beat zimekua za kisasa zaidi, cranky na nini. Kuna aina nyingine ya mashabiki wetu tunahitaji kuwa nao karibu pia” aliongeza. Mansu-li amesema kwamba ameona kutoa nyimbo hiyo itafanya kitu cha tofauti kidogo. Kama ulipitwa na nyimbo hiyo.


Unaweza kuisikiliza hapa:mdundo.com/song/51404

 

Leave your comment