TANZANIA: Almasi aibuka na ‘Baishoo’
18 April 2016

Tasnia ya mziki wa Bongo fleva unazidi kukua na kuibua vipaji vingi kutoka kwa wasanii chipukizi, Leo tulifanya mahojiano na Almasi Amiri jina la usanii ni Almasi masound.
Almasi masound ni kijana ambae hivi sasa ametoa video yake mpya inayokwenda kwa jina la Baishoo, video ambayo imefanywa na Director Deo Abel chini ya uongozi wa Sweseka Production. "Mziki ulikuwa una nafasi kubwa sana katika maisha yangu kuliko shule, kwasababu mziki mimi nilianza kuimba tangia nikiwa Form one huko kigoma" Alisema masound
Katika kipindi chake cha mziki, Almasi alishafanya ngoma tatu ambazo alizifanya alipokuwa Kigoma huku akipewa sapoti kubwa kutoka kwa Sentano records.
"Nilishafanya nyimbo tatu ambazo zilikuwa ni NIKUIMBIE, MY na NITUNZE hizi nilizifanya kupitia studio ya Sentano records pamoja na Grey bakuza records" aliendelea kueleza. Almasi kwa sasa yupo chini ya Sweseka production ambao ni wamesimamia ujio wa ngoma na video ya Baishoo.
Unaweza kuitazama video hii hapa:




Leave your comment