TANZANIA: Idris ajiunga na Fezza Kessy Choice Fm

Mshindi wa mashindano ya Big Brother Africa, Idris Sutan amejiunga na msanii wa bongo fleva nchini Tanzania, Fezza Kessy katika kituo cha utangazji cha Choice Fm ambayo iko chini ya usimamizi wa Clouds Media.

Redio ya Choice Fm katika ukurasa wao wa Instagram wamepost na kuandika:

Karibu @idrissultan kwenye usajili mpya wa 102.5 Choice Fm kwenye kipindi cha #HardDrive kuanzia saa 12-3 asubuhi.
Idriss ataungana na Feza Kessy katika kipindi hiko cha Hard Drive kuanzia saa 12 hadi saa 3 asubuhi. Mbali na hao pia kuna Dj Sinyorita pamoja na Mami ambao wote walikuwa katika kituo cha utangazaji cha Ea Radio na kuhamia Clouds.

 

Leave your comment