TANZANIA: ‘Wivu ndio kila kitu’ - Linex

 

Msanii Linex amefunguka kuhusu mpenzi wake wa sasa na kukiri kuwa ni mapenzi mabaya hasa ukiwa na yule anayekupenda.

Akiongea kwenye kipindi cha E-news kinachorushwa na East Africa Television, Linex amesema ukishakuwa kwenye mapenzi, lazima masuala ya wivu yatakuwepo na hicho ndicho kipimo cha mapenzi kwa yule mwandani wako. “Mapenzi mabaya means kwamba ukishakuwa kwenye mapenzi, mpenzi wako akikuonesha wivu kuhusiana na jambo fulani ambalo hajalielewa, huwezi 'kumdoubt' unatakiwa ufurahi kumbe napendwa mimi”, alisema Linex

Pia Linex amesema ili kujiepusha na migogoro na mwenzi wake huyo ambaye amemuweka wazi kwa jamii, amesema wao kama wasanii anachofanya ni kujiepusha na mitandao ya kijamii kuchunguza nini anafanya kwani mwenzi wake huyo hamchunguzi kwenye mahusiano.
“Kwa mfano mimi ngoja nikwambie kitu kimoja, mimi simfollow wala yeye hanifollow, hajui ninachopost wala sijui anachopost”, alibainisha Linex kuhusu yeye na mpenzi wake.

 

Leave your comment