TANZANIA: Diamond aongelea reality show yake

 

Msanii wa muziki wa nchini Tanzania anayefanya vizuri, na kuitambulisha vyema muziki wa bongo fleva ndani na nje ya mipaka ya Afrika kwa nyimbo zake kama ‘Mdogo Mdogo’, ‘Utanipendaga’,’Mbagala’ na nyinginezo nyingi. Hivi karibuni staa huyo alikuwa na safari za nchi za nje  kama vile Sweden, Belgium, Finland, USA, Norway pamoja Germany na kumfanya kukua zaidi na zaidi. Katika mahojiano yake na kituo cha Clouds Media Diamond amesema ana mpango wa kutoa reality show na si Kireality show.

Akiongelea kuhusu hilo Diamond anasema, “ sio tu bora reality, ni reality bora, na watu wamekuwa wakisubiria kwa muda mrefu  mbali na hiyo pia hata mimi nilitani kuifanya kwa muda mrefu kuna vitu vikamilike , kama production ukizungumzia production, kuwa na content za kutosha, na kupata sponsor mkubwa ambae ataweza kuingiza hela nyingi”.

“Bao vitu vidogo tu kitu kipakuliwe, itakuwa ni online pamoja na kwenye tv, sema exclusive itaanzia kwenye moja ya mitandao”, aliongeza Diamond.

 

 

 

 

 

 

Leave your comment