TANZANIA: Tunampango wa kuongea na menejimenti ya KanyeWest - Babutale
11 April 2016

Meneja wa Diamond Platnumz Babutale amesema kuwa siku walivyokutana na Kanye West hawakuishia kupiga picha tu, mengi yaliongelewa. Katika mahojiano yake katika kipindi cha Playlist cha 100.5 Times Fm Babutale alisema, siku ambayo Diamond Platnumz alipata bahati ya kupiga picha na msanii huyo wa kimarekani Kanye West, Babutale alidai kuwa Kanye West alimfuata Diamond kwa nia ya kupiga picha kiatu chake alichokua amekivaa. Na ndipo Diamond alipomuangalia vizuri na kumuona kuwa ni Kanye West na kuomba kupiga nae picha.

Babu tale alisema kuwa kabla ya kupiga picha hizo walijaribu kuongea nae mambo mawili matatu. “Tuombe Mungu , tumeweza kupata ukaribu na menejimenti yake , kila kitu kitawezekana. Tupo kwenye mazungumzo ya katikati hayajafika mwisho”, alisema Babutale.




Leave your comment