TANZANIA: “Imeniuma sana video ya Wema” – Idris
11 April 2016

Idris Sultan afunguka baada ya video iliyomuonyesha wema sepetu akimbusu mwanaume mwengine. Katika mahojiano yake Idris Sultan na mtangazaji Larry Madowo wa kipindi cha The Trend cha nchini Kenya, Idris alisema kuwa video aliyosambaa katika mitandao ya kijamii iliyomuonyesha mpenzi wake Wema Sepetu akimbusu mwanaume mwingine ilimuuma sana.

Idris akiwa na mtangazaji wa The Trend Larry Madowo
“Ingetoka kwamba tuko kwenye party na huyo jamaa ‘Gay’ najua wakati mwingine ni kitu cha mchezo kumbusu mwanaume Gay haijalishi, wao ni nyoka wasio na sumu lakini inapotokea unapuuza tu”, amesema Idris.
“Lakini pale video inapowekwa mitandaoni na anaiongelea na kuja kwangu na kusema , mwanamke wako anachukuliwa na huwezi kufanya chochote sasa wanaanza kuniita bwege. , huwezi hata kumtawala mwanamke wako, unashindwa kumkataza kufanya hili na lile. ila ninapojaribu kuongea nae hanijibu vizuri. Niliongea nae na akaniletea kiburi, alipokuwa hivyo nikasema nilitaraji ungeelewa. Sijiskii vizuri kuhusu hili . Najisikia vibaya kwani si kwasababu ya busu bali ni kwasababu iko mtandaoni, ni chuki kiasi gani ninazozipata kutokana na hili”, alisema Idris.
Idris alisema kuwa mwanzo alipoona video hiyo alijua ni utani wa siku ya wajinga duniani, “ Na kisha nikagundua kuwa huu si utani, inaumiza”.
Unaweza kuangalia mahojiano hayo hapa:




Leave your comment