TANZANIA: Nilifukuzwa kwenye nyumba mimi – Maua Sama

 

Msanii anayetamba na kibao kama ‘Mahaba niue’ na ‘Siwezi’ amesema kwamba alishawahi kufukuzwa kwenye nyumba. Hayo aliyasema Maua katika mahojiano yake na Millard Ayo hivi karibuni nakusema kuwa kitu ambacho hatakuja kukisahau ambavyo pia vilikuwa ni vikwazo katika safari yake ya muziki ni mara baada ya kufukuzwa kwenye nyumba.

“Kuna kipindi nilikuja Dar sehemu niliyofikia, ni kwa mtu ambae alinikaribisha kwake lakini hakumwambia mwenye nyumba wake. Wenye nyumba alinifukuza, kidogo anifungulie mbwa”.

“Nilipotoka hapo kuna duka nje niliweka vitu vyangu then nikaondoka. Nilienda Mj records nikakaa nikavunga nikapiga nao stori mpaka usiku Sajo akanifwata akanipeleka nyumbani kwake”.

 

 

Leave your comment