TANZANIA: Belle9 aeleza matunda ya menejimenti yake mpya

 

Msanii anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki hapa nchini Tanzania na anaetamba na kibao cha ‘Burger Movie Selfie’, Belle 9 amesema kuwa menejiment yake inampa fursa ya kufanya vizuri.

Hapo mwanzo msanii huyu hakuwa na menejiment, katika mahojiano yake na Millard Ayo Belle9  alisema kuwa  muda wake umefika wa yeye kuwa na menejiment. “Kwa mara ya kwanza ngoma yangu ya ‘Shauri zao’ imechezwa Trace, hakuna video yangu lishawahi kupata hiyo nafasi. Na pia nimekuwa Brand Ambassador, sikuwahi kuwa Brand Ambassador huko nyuma”, alisema Belle 9.  Belle9 amekuwa Brand Ambassador wa OBAS.

Belle9 amesema kuwa mipango yake ya mwaka huu 2016 ni kuutoa muziki pale uipokuwa na kupeleka mbele zaidi.

 

 

 

 

 

Leave your comment