TANZANIA: Alikiba azua utata kuhusiana na Jokate

 

 

Ukimya wawekwa wazi, ni kuhusu tetesi za msanii anayefanya vizuri nchini AliKiba pamoja na aliyekuwa Miss Tanzania na kushika nafasi ya tatu mwaka 2006  ambaye pia ni mwanamitindo, Jokate Mwegelo, ambaye inasemekana yupo naye kwenye mahusiano ingawa mwenyewe anakanusha. Akiongea kwenye kipindi cha eNews kinachorushwa na East Africa Television, Ali Kiba amesema siku hizi watu wanasahau na kudharau waliyokuwa wakiyafanya wazee wetu katika kuchagua mke wa kuoa.

 

 

 

 

“Unajua siku hizi watu wanasahau kuwa wazee wetu walikuwa wanachagua vipi msichana, siku hizi tunaoana tu, unaishi nae miaka mitatu, lazima muwe marafiki, hivyo ni vigumu kuachana na rafiki, ila ni rahsi kuachana na mpenzi wako”, alisema Ali Kiba. Pia ameendelea kusisitiza kuwa yeye na Jokate ni marafiki tu na sio wapenzi kama watu wengi wanavyodhani na kuibua maswali yenye utata kuhusu kauli yake ya kwanza aliposema "Unapooa, lazima muwe marafiki na huyo mwandani wako, ili kudumisha ndoa yenu".

 

 

 

Leave your comment