TANZANIA: “Kwa Shilole nilikuwa nikifanya mapenzi sio muziki” – Nuh Mziwanda
5 April 2016

Aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Shilole Nuh Mziwanda amefunguka mna kusema kuwa, kwa shilole alikuwa akifanya mapenzi na wala hakuwa akifanya muziki. Akizungumzia katika kipindi cha Clouds E Jumatatu hii alisema hali hiyo ilimfanya apotee kimuziki na kukiki zaidi kimapenzi.
“Kwa Shilole nilikuwa nikifanya mapenzi sio muziki, ndio maana ukakona kwenye muziki sikuwa vizuri. Hata followers wetu walikuwa wanakuja kuangalia mapenzi n a sio kwa ajili ya muziki. Ndio maana alikuwa anashindwa kunishauri kuhusu muziki wangu, kwa maana kama angekuwa ni mtu sahihi angekuwa akinishauri kwenye maswala ya kujenga”, alifafanua Nuh. Kwa sasa Nuh amejipanga kuachia ngoma zake za kuimba pamoja na kurap.
Chanzo: Bongo5




Leave your comment