Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Ray C alinisaidia – Babu Tale
4 April 2016

Meneja wa Tip Top Connection na WCB, Babu Tale, amefunguka kuwa anatamani kumsaidia Ray C kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya na kumrejesha vizuri kwenye muziki kama zamani kwakuwa naye aliwahi kumsaidia. Akiongea kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM, Jumamosi iliyopita, Tale alidai watu wengi hawajui Ray C alimsaidia kwa kiasi kikubwa kukaa kwenye ramani nzuri kisanaa kama alivyo leo.
“Natamani sana kumsaidia Ray C, natamani mno, zamani nilikuwa naigiza sauti za watu hata mia, ikaenda kipindi hicho Ray C anafanya kazi East Africa nilikuwa nafanya naye mi kazi yangu ilikuwa kugeza sauti, wakina mzee Msekwa nini,” alisema Tale.
“Na mimi ndiyo nilimchukua Babu Ayubu, sikuwahi isema hii, sijaonana naye ila nimepanga ndani ya siku hizi mbili nione namna ya kumsaidia,”aliongeza.
Tale aliongeza kuwa imefika wakati Tanzania kijengwe kituo maalum (rehab) kwaajili ya watu maarufu ambacho wasanii na watu maarufu wengine watakuwa hawachanganywi na watu wa kawaida.
Chanzo: Bongo5
Weekly Top 10 songs

Black Mark utandilubi omwami wangu5:21
KAPEKE LONDON2:23
In My Bed2:50
Paver2:55
CHAMPION GAL3:00
Ex Nkubilako ft DonMusa2:55
BIkola2:58
The Prelude of Grace1:31
Joy Is Coming3:08
Worship My King5:00


Leave your comment