TANZANIA: Aslay amzungumzia mzazi mwenzake na umeneja..

 

Aslay ni muimbaji kutoka kwenye kundi la Ya Moto Band, kilichomfanya awepo kwenye post ni kauli yake ya kukanusha ya kumtelekeza msichana mwenye ujauzito wake na aliyeishi nae kwa muda wa kipindi cha miezi sita. Aslay mwenye umri wa miaka 20  amesema, “Baada ya kuishi pamoja miezi sita,tulizinguana na kuamua kila mtu akaishi na hamsini zake, sisi vijana bwana mambo mengi… tukaangalia pia mimi umri wa kuishi na mwanamke bado, na yeye umri wa kuishi na mwanaume bado”

 

 

 

‘Sikuchukua uamuzi ila wote ndio tulichukua uamuzi…. nilimuacha na ujauzito wangu na tayari amejifungua mtoto wa kike ambaye ana kama mwezi mmoja na nusu, mwanangu nimemuita Moza jina la marehemu mama yangu… na bado mpaka sasa tunaonana hata hapa nimetoka kumuona mwanangu, hatujarudiana…. tunashirikiana tu kama mtu na mzazi mwenzake‘ – Aslay

Kingine alichokiongea Aslay kwa sasa ni kwamba amekabidhiwa majukumu mapya ya kuwa meneja, aliyemkabidhi ni boss wake Mkubwa Fela kiongozi wa Mkubwa na Wanawe na sasa Aslay ni meneja wa madada watano aliokabidhiwa miezi mitatu iliyopita na watasikika very soon.

 

Chanzo: Millardayo.com

 

 

Leave your comment