TANZANIA: AliKiba awapa nafasi mashabiki kutoa jina la wimbo wake mpya.

 

 

 

Alikiba awapa nafasi mashabiki wake kumpa jina la wimbo wake mpya anaotarajia kuutoa hivi karibuni. "Mashabiki zangu kaeni mkao wa kula nashusha balaa lingine muda si mrefu kutoka sasa. Hii ngoma hata sijui mimi niiiteje yaani ila nitawaachia wenyewe wananchi mchague jina la kazi hiyo" alisema Ali Kiba katika mahojiano yake na kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na kituo cha utangazaji cha East Afrika Radio.

Mbali na hilo Ali Kiba amesema kuwa kitendo chake cha kutoa wimbo bila video kimekuwa na athari kubwa kwake kwani wimbo unakuwa mkubwa na mashabiki wanakuwa tayari na video zao vichwani mwao, kiasi kwamba anapokuja kutoa video ya wimbo huo unakuwa tofauti na mategemeo na matarajio ya baadhi ya watu jambo ambalo huwa linaleta maneno maneno.

 

 

Leave your comment