TANZANIA: ‘Dili nililopata Marekani lilinisababisha ni nyoe ndevu’ – Ben Pol
4 April 2016

Mwanamuziki anaye kimbiza kwenye miondoka ya Rn'B, Ben Poul, amedai kuwa ndevu zake ambazo aliziwekea hina upande mmoja aliamua kuzinyoa kwa kuhofia kuonekana kuwa yeye ni mmoja wa wanamgambo wa makundi ya kigaidi.
Ben Poul ameyazungumza hayo alipo fanya mahojiano ndani ya Friday Night Live, show inayorushwa na East Africa Television nakusikika pia kupitia East Africa Radio, ambapo amesema deal la kufanya kazi na Wamerekani alipo lipata lilimsababisha anyoe ndevu zake ambazo zilisha kuwa ndefu na kudhani angeonekana mmoja wa washirika wa ugaidi ikiwemo kundi la Al Qaeda.
Mara ya Mwisho Ben Pol aliposhiriki show ya Friday Night Live alifunguka kuwa ameamua kuwekea ndevu zake hina kwakuwa hana wazo la kusuka wala kujichora tattoo hivyo kwake itakuwa ni kama kitambulisho chake Ila kwa sasa ameamua kuzibadilisha na kuwa kawaida.
Chanzo: Enewz.com




Leave your comment