Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Uchawi upo kwenye muziki – Mkubwa Fella
4 April 2016

Meneja wa Kundi la Yamoto Band Said Fella ‘Mkubwa Fella’ amesema anakubali kwenye tasnia ya muziki hapa nchini uchawi pia upo. Fella ameyasema hayo katika kipindi cha eNews kinachorushwa na EATV siku ya Jumatano baada ya msanii wa bendi ya Jordan inayopiga nyimbo za injili kusema kwamba kwenye muziki wa Bongo Fleva masuala ya ushirikina yapo sana.
''Ukimtumikia Mungu unakuwa hata ukipata hela yako unajua unaifanyia nini na inakuwa inadumu lakini ukitumikia muziki wa kidunia wengi wanalogana na ndiyo maana mtu anavuma kidogo baada ya muda anapotea kabisa''-Amesema Daniel wa Jordan Band.
Katika kupima kauli hiyo kama ina ukweli ndani yake mtayarishaji wa eNews akaamua kumsaka Diwani wa Kata ya Kilungule Wilayani Temeke Jijini Dar es salaam Said Fella ambaye pia aliunga mkono kauli hiyo.
Weekly Top 10 songs

Black Mark utandilubi omwami wangu5:21
KAPEKE LONDON2:23
In My Bed2:50
Paver2:55
CHAMPION GAL3:00
Ex Nkubilako ft DonMusa2:55
BIkola2:58
The Prelude of Grace1:31
Joy Is Coming3:08
Worship My King5:00


Leave your comment