TANZANIA: Kashfa za wasanii kutumia madawa ya kulevya inawachafua wasanii - AY

 

Ambwene Yesaya ‘AY’  amesema kukithiri kwa madawa ya kulevya  kwa wasanii wa kizazi kipya nchini kutashusha soko la wasanii hao kwa kukosa uaminifu. Akizungumza na gazeti la Mtanzania Alhamisi hii, AY amesema kuwa hizi kashfa za wasanii kutumia madawa ya kulevya inawachafua wasanii wa mataifa mbalimbali ili kukuza uchumi badala ya kushirikiana katika matumizi ya madawa ya kulevya.

“Kinachotakiwa kwa sasa, wasanii watumie fursa za kushirikiana na wasaniiwenye mashabiki wengi toka nje ya nchi ya nchi kwa ajili ya kujiongeza mtandao, soko na fedha zaidi, sio kujiingiza katika matumizi ya uuzaji wa dawa za kulevya”, alifafanua AY.

 

Chanzo:Bongo5.com

 

 

Leave your comment